Watu 4 na wengine 29 Wajeruhiwa Baada ya Basi la HBS Walilokuwa Wakisafiria Kupinduka Jijini Mbeya

Basi hilo likiwa limebeba abiria wengi kuliko uwezo wake, lilianza
safari yake ya kuelekea Tabora likitokea jijini Mbeya, lakini inadaiwa
kuwa likiwa kwenye mtelemko na kona kali za mlima Mbeya likafeli breki
na ndipo dereva wake akaamua kuruka na kuliacha likijiendesha lenyewe
hali ambayo ilisababisha lipoteze mwelekeo na kuanguka mtaroni.
Muuguzi
wa zamu katika hospitali ya rufaa ya kanda ya nyanda za juu kusini,
Jesca Kahangwa amethibitisha kupokea miili ya watu wanne na majeruhi 29
wa ajali hiyo, huku akidai kuwa hali za majeruhi wengi bado ni mbaya.
Mwenyekiti
wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amewahi
katika eneo la ajali na baada ya kupata maelezo ya chanzo cha ajali
hiyo, akaliagiza jeshi la polisi kuwatafuta na kuwakamata haraka dereva,
kondakta na mmiliki wa gari hilo kwa kosa la kuendesha gari bovu
barabarani.


Hakuna maoni