Master J awaomba wasanii waache kudharau maproducer.


Producer mkongwe na mmiliki wa lebel ya Mj Records Master J ametoa hisia zake juu ya wasanii wanaochukulia powa maproducer wa bongo kwa kuwalipa pesa kidogo huku wao wakichukua pesa ngingi kwenye show na kulipia video pesa nyingi zaidi.
Master J amesema “Sio sawa kumsikia msanii anasema video nimelipia dola elfu thelathini, huku audio katoa laki au laki mbili, hii ni dharau sana, wasanii waache hili jambo”
Jay pia amesema alijaribu kuongea na mameneja wakubwa wa muziki bongo na walikata kuunga mkono harakati hizi wakidai kuna sehemu wanaweza hata kurekodi bure.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.