Rufaa ya kupinga kuachiwa Zombe na wenzake imesikilizwa leo April 29 2016


Mahakama ya Rufaa imesikiliza rufaa ya kupinga kuachiwa huru kwa aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es salaam ‘RCO’ Kamishna Msaidizi wa Polisi ‘ACP‘ Abdallah Zombe na askari wenzake watatu waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka ya mauaji.
Rufaa hiyo imesikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu ambapo wamesikiliza pande zote mbili wa mashitaka na utetezi na itatoa maamuzi baada ya majaji kupitia kesi hiyo.
Mkurugenzi wa Mashitaka ‘DPP’ alikata rufaa mwaka 2013 akipinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam iliyowaachia huru Zombe na wenzake baada ya kuwaona hawana hatia katika kesi ya mauaji ya watu wanne iliyokuwa inawakabili.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.