Hafsa Kazinja karudi Sekondari…
.
Star wa hit single ya Presha Hafsa Kazinja
ambayo alimshirikisha mkali mwingine kutoka B Band maarufu kama Banana
Zoro leo alimplify sababu zilizopelekea kuwa kimya kwenye tasnia ya
muziki wa Bongo Fleva.
Akizungumza leo June 26 kwenye AMPLIFAYA ya Clouds FM alisema...’Of
course nipo kimya kwenye maradio ila matamasha nafanya kama kawaida
naweza nikawa kimya kwenye media lakini kazi zangu bado zinatambulika
nje na ndani ya nchi kwa hiyo bado nafanya, lakini kitu ambacho naweza
sema kwanini niko busy sasa hivi niliamua kurudi shule kwahiyo nilirudi
shule mwaka jana kwa hiyo inataka moyo sana kuanza form one,form two ni
(QT) kwa hiyo mwaka jana Mungu akanijalia nikafaulu masomo yangu ya form
1 & 2 sasa hivi niko form 4 nasubiri nimalize maana mtihani wa form
4 sio mchezo
Kwa hiyo pamoja huku nasoma pia nina wimbo wangu mpya siwezi kuuzungumzia ila bado upo katika matayarisho yaani studio’alisema
Unaweza uka bonyeza play kumsikiliza Hafsa Kazinja
Hakuna maoni