Barua ya Mfungwa Papii Kocha kwa Rais JK.


 
BARUA YA PAPII KOCHA KWA RAIS JAKAYA KIKWETE... KWA WALE AMBAO HAMJAISOMA HÍI HAPA.MF/NA: 836'04
 
Johnson Nguza (Papii Kocha)
Gereza Kuu Ukonga
S.L.P 9091
Dar es Salaam
Mh. Rais Jamuhuri yaMuunganoTanzania
YAH: MAOMBI YA KUPEWA MSAADA(MSAMAHA) WA KUFUTIWA ADHABU
YA KIFUNGO NILIYOPEWA NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU.

Husika na somo hilo hapo juu.Mimi ni mfungwa katika gereza kuu Ukonga. Kwa heshma
na taadhima na kwa kutambua utuna huruma yako yakiMUNGU ulionayo dhidi ya
binadamu  wenzako pamoja na mamlaka uliokabidhiwa na Jamuhuriya
Muungano wa Tanzania. Naanguka na kushikamiguu yako mitukufu muheshimiwa rais.
Nakuomba msaada(msamaha)kwako muheshimiwarais, kwa njia hii ya maandishi
kusudi niweze kuondolewa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani,niliyohukumiwa
na mahakama tajwa hapo juu. Mh.Rais mimi nimefungwa nikiwa bado kijana mwenye umri
mdogo,na ukweli kutoka moyoni sikufanya kosa hilo. Si mimi, baba yangu Nguza wala ndugu
yangu yeyote aliyefanya kitendo kile. Lakini wenye mamlakawakatuona tuna hatia na kuamua
kuteketeza kizazi chetu gerezani. Natamani kiama ifike ili mwenyezi Mungu aweke wazi
ukweli wote uliojificha nyuma ya pazia. Mpaka sasa natambua wazi
hatima pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono
yako mitukufu Mh. Rais Naomba huruma yako muheshimiwa Rais
maana mimi ni mtoto wako ninaehitaji huruma yako wewe mzazi. Lakini pia sisi
ni binadamu wenye nafsi na miili kama wengine. Waliotumia mamlaka yao
kutuweka gerezani nao ni binadamu pia, wenye miili na nafsi. Ipo siku nafsi zetu zitapaswa kutoa hesabu ya tuliyoyafanya hapa duniani. wakati huo miili yetu tunayoitumia kunyanyasa wanyonge itakuwa imeozamavumbini. Natumaini kauli yako ya mwisho ndio itakayoleta pumzi ya
uhai nafsini mwangu. Nakutakia kazi njema, afya njema na
maisha marefu. Mungu akubariki. Wako mtiifu
Mfungwa NO:836'04
JOHNSON NGUZA (PAPII KOCHA)

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.