Ronaldo atishia kuondoka Old Trafford, United ikishindwa kufuzu Champions League
Wawakilishi wa Cristiano Ronaldo wameiambia Manchester United kwamba mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 36 anapania kuondoka Old Trafford msimu wa joto ikiwa klabu hiyo itashindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Kwa mujibu wa The Sun, wameeleza wasiwasi wao kuhusu kushuka kwa kiwango cha klabu hiyo. Ronaldo amebaki “amechanganyikiwa” na “akiwa na wasiwasi” na hali ya sasa ya Old Trafford na ataondoka mwishoni mwa msimu kama klabu hiyo itafeli kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa.
Hakuna maoni