Wanajua tupo katika kipindi kigumu – Pablo Franco kuhusu Simba Vs Dar City


Kocha wa Mabingwa watetezi kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) Simba SC, Pablo Franco amesema kuwa wapinzani wao Dar City wanafahamu kuwa Simba ipo kwenye kipindi kigumu hivyo watataka kuwapa hofu kwenye mchezo wa leo lakini wao wapo tayari kuwakabili.

”Mchezo utakuwa mgumu, wapinzani hawana cha kupoteza na wanajua tupo katika kipindi kigumu, kwa hiyo watataka kutupa hofu ili kututoa mchezoni, lakini tupo tayari kuwakabili.”- Pablo Franco

Simba ambaye ndiyo Bingwa Mtetezi wa michuano hii ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) watashuka uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 jioni kuwakabili Dar City.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.