MSIBA WA MWENYEKITI BONTA WA DURBAN TACOSA


Habari ndugu zangu, kwa moyo wenye majonzi makubwa naendelea kutoa taarifa ya msiba mkubwa kwa ndugu zetu wa Durban, KZN na Watanzania wote.

Ndugu yetu Bonta, umauti umemkuta leo mapema, 21 January 2022 baada ya kupata na ugonjwa wa muda mfupi.

Naomba nimuongelee kidogo *Mwenyekiti wa Kwa Zulu Natal*

Mimi binafsi namuita mwenyekiti wa  KZN kwani hakuna tatizo linalotokea KZN na kama hakuna mtu basi alikuwa tayari kusafiri sehemu yoyote bila hata kuuliza Mara mbili.

Mwenyekiti alikuwa na tabia zake hakutaka mtu anayeongea haraka haraka au shuruti ila kama tatizo ni la Mtanzania basi jua atalifuatilia hata kwenye mazingira magumu au hatarishi.

Binafsi nimepoteza jembe la nguvu kwa upande wa KZN na kiunganishi kwa Watanzania wa hali zote kuanzia mabaharia wa Beach mpaka maprofesa wa vyuoni.

Kama kuna tuzo za uongozi bora basi kaka Bonta anastahili tuzo hiyo kwa kujitoa kwake katika mambo mbalimbali ya kijamii ya Watanzania wa KZN. 

Simpambi kwa kuwa ni marehemu ila kwa wanaomjua watakubaliana na mimi. Wakati wa machafuko yote ya Durban kaka Bonta atakupa ripoti ya kila jambo linalotokea KZN sio Durban tu. 

Kwa kweli tumeondokewa na kiongozi muhimu sana katika jamii na jumuia yetu ya Watanzania. 

Kwa niaba ya viongozi wa TACOSA na jumuia zote za Watanzania tunapenda kuwapa pole familia yake ya Tanzania na hapa Afrika Kusini, ndugu, jamaa na marafiki wake wote na wote walioguswa. 

Bado maandalizi ya mazishi yanaendelea katika familia na tutapata taarifa zaidi na kuzituma hapa. 

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. 

*Hamba kahle Qawe Bonta*

Alex Minja 
Katibu TACOSA 
21 January 2022

Maoni 1 :

Inaendeshwa na Blogger.