Korea Kaskazini yafanya jaribio jingine la kombora

Korea Kaskazini imerusha kombora jingine baharini mashariki ya pwani yake. Tukio hilo limeripotiwa leo na serikali za Korea Kusini na Japan.

Mkuu wa majeshi ya Korea Kusini amesema kombora hilo lilikuwa la masafa ya umbali wa kilomita 800. Msemaji wa serikali ya Japan Hirokazu Matsuno ametaja tukio hilo kuwa kitisho kwa Japan na Jumuiya ya Kimataifa.

Korea Kaskazini imekuwa ikizidisha majaribio ya makombora katika siku za hivi karibuni, tukio hili likiwa la saba katika mwezi huu. Mnamo Alhamisi, Pyongyang ilirusha makombora mawili ya masafa mafupi baharini.

Nchi hiyo imepigwa marufuku na Umoja wa Mataifa dhidi ya majaribio ya makombora na zana za nyuklia. Taifa hilo pia lilijaribu makombora ya masafa marefu siku ya Jumanne huku likiapa kujiimarisha zaidi kinyuklia na kutengeneza silaha zenye nguvu zaidi.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.