Rais Samia atuma salamu za pole kufuatia kifo cha kaka wa makamu wa rais Dkt. Philip Mpango
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana, Gerald Mpango ambaye ni kaka yake Mhe. Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango.
Rais Samia ametuma salamu hizo kupitia ujumbe wake kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram ya Ikulu
”Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana, Gerald Mpango ambaye ni kaka yake Mhe. Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango. Pole kwa Kanisa, familia, Mhe. Makamu wa Rais, ndugu, jamaa & marafiki. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina.” – Rais Samia
Hakuna maoni