blogger-disqus-facebook
  • About
  • Contact Us
  • Home

kazikazi_newsupdates

Breaking News | International News | Political | Business | Sports | Games | Entertainments | Global Music | East Afrika | Bongo Flavour | Bongo Movie | Udaku wa Social Media

kazikazi_newsupdates
    • NEW VIDEO
    • KAZIKAZI TV
    • SAUTI ZA MITAANI
    Home / Unlabelled / Bei Kubwa Vifurushi vya Data Tanzania Mwiba wa Maendeleo ya Kidigital 5

    Bei Kubwa Vifurushi vya Data Tanzania Mwiba wa Maendeleo ya Kidigital 5

    Mwandishi Mchapa kazi Novemba 09, 2021 0


    Wadau walia kila kona vifurushi kupanda maradufu tena kimya kimya

    Tasnia ya habari Mitandaoni, elimu, Dini, Burudani waathirika pakubwa*

    Kutokana na kupanda maradufu kwa bei za vifurushi vya interneti nchini, huku GB 1 ya Data ikipatikana kwa zaidi ya dola 1.3 kumesababisha kupungua kwa kasi idadi ya watumiaji wa internet nchini hivyo kuathiri taasisi, mashirika na watumiaji binafsi wa interneti ambao hutumia huduma hiyo katika majukumu mbalimbali pamoja na burudani.

    Aidha, kutokana na bei hizo kutokuwa rafiki kwa watumiaji wa huduma hiyo hasa mwananchi wa kawaida Taasisi na tasnia mbalimbali zimetajwa kuathirika kwa namna moja au nyingine

    *Tasnia ya habari za kidigitali*
    Watoa huduma za maudhui katika Tovuti na programu tumishi na mtandao wa YouTube na blogs wamelalamika kutokana na kushuka kwa kasi kwa watumiaji wa huduma zao huku wakiiomba wizara na wadau husika kujadili na kulipatia mwarobaini suala hili.

    Ili kuendesha mitandao ya kijamii inatakiwa kutumia bando kila wakati ili kuendelea kuuhabarisha umma kuhusu habari na matukio mbalimbali hivyo gharama kubwa za vifurushi zimekuwa kikwazo kwa bloggers & youtubers.

    *Tasnia ya Burudani*
    Wasanii na watoaji maudhui ya burudani hasa kwa mtandao wa video wa YouTube nao wamedai idadi ya wanaofuatilia kazi zao kushuka kwa kasi kwa siku za karibuni, jambo ambalo wamedai kuathiri sana kipato chao. Vilevile mitandao mbalimbali ya takwimu inaonesha kushuka kwa watumiaji wa mtandao wa YouTube Tanzania kwa siku za karibuni.

    *Watumiaji Binafsi*
    Watumiaji mbalimbali wa internet Tanzania nao wameonesha kukerwa na kupanda Mara kwa Mara kwa bei za vifurushi tena vinapandishwa kimya kimya licha ya mamlaka kusema gharama zimeshuka huku wakidai uishaji wa haraka kuliko kawaida wa vifurushi hivyo, vile vile wanakumbusha ahadi za wadau na wizara kuahidi mara kadhaa kulishughulikia tatizo hilo na kubakia ahadi hewa.

    Pamoja na hayo, Bei hizi ambazo zimetajwa kutokuwa rafiki kwa watumiaji huenda zikazidi kuathiri mfumo mzima wa maendeleo ya kidigitali hasa kwa mashirika, taasisi, na makampuni kama vile huduma za kibenki za kidigitali, huduma za afya, elimu, na dini zinazopatikana kwa njia za kidigitali pamoja na tasnia ya michezo ya bahati nasibu ya mtandaoni.

    *Haki ya kupata taarifa, imeathiriwa*
    Kila mtu ana haki ya kupata taarifa, kwa miaka ya karibuni kutokana na ukuaji wa maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano hata Serikali imekuwa ikitoa taarifa zake kwa idara mbalimbali kwenda kwa wananchi kwa njia ya mitandao, hii inahusisha hata Matangazo ya moja kwa moja ya Uapisho wa viongozi, uzinduzi wa miradi na hotuba za viongozi kwa wananchi ambao wapo maeneo tofauti tofauti. Kutokana na kupanda kwa gharama za bando baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanakosa haki ya kupata taarifa hizo kutokana na bando kupaa.

    Hapo awali ilikuwa rahisi mtu kuweza kufatilia mubashara matangazo mubashara ya matukio ya kitaifa kupitia mtandaoni lakini hivi sasa wananchi wengi tunapata shida kuweza kuangalia hadi mwisho matangazo hayo kwani maranyingi kabla tukio halijaisha kifurushi cha data kinakuwa kimeshaisha, hivyo athari hizi si tu kwetu wananchi ila hata kwa watoa taarifa wakiwemo viongozi wa Serikali.

    Na hivyo ujumbe uliokusudiwa kuwasilishwa kwetu wananchi unakuwa umekwamishwa na gharama za vifurushi vya data.

    *Wadau Watoa ushauri*
    Wadau mbalimbali wanaishauri wizara husika, pamoja na makampuni ya simu nchini yanayotoa huduma hiyo muhimu kwa maendeleo kuangalia upya na kwa umakini jambo hili kwa maendeleo na tija ya nchi.

    Tunafahamu kuwa Vifurushi vya Data ni Ofa za makampuni ya simu katika kufanya ushindani wa kibiashara lakini licha ya kuwa ni ofa basi tunashauri ziwe zenye kuleta unafuu kwa mwananchi kwakuwa pia kukiwa na huduma hizo nzuri, hata matumizi ya Mawasiliano kwa njia ya simu yataongezeka na kutaongeza mapato kwa Serikali kwa njia ya kodi na tozo zilizopo hivi sasa.

    *Imeandaliwa na baadhi ya watoa maudhui, waandishi wa habari za mtandaoni na watumiaji wa mitandao Tanzania*
    Tags:

    Hakuna maoni

    Jisajili kwenye: Chapisha Maoni ( Atom )

    Kazikazi Digital

    Kazikazi Digital
    Let Us Host your Business and Bost it to the Higher Level

    kazikaziTv

    kazikaziTv
    News Updates in Politics, Sports, Entertainment, Education
  • Recent

    3/recent-posts

    Comments

    3/recent-comments

    Facebook

    SAUTI ZA MITAANI SHOWS

    TRENDING MUSIC VIDEO

    Kumbukumbu la Blogu

    • ►  2024 (6)
      • ►  Desemba (1)
      • ►  Oktoba (1)
      • ►  Januari (4)
    • ►  2023 (25)
      • ►  Desemba (1)
      • ►  Novemba (1)
      • ►  Septemba (1)
      • ►  Agosti (2)
      • ►  Mei (2)
      • ►  Aprili (5)
      • ►  Machi (4)
      • ►  Januari (9)
    • ►  2022 (242)
      • ►  Desemba (3)
      • ►  Agosti (4)
      • ►  Julai (4)
      • ►  Juni (15)
      • ►  Mei (37)
      • ►  Aprili (13)
      • ►  Machi (31)
      • ►  Februari (53)
      • ►  Januari (82)
    • ▼  2021 (296)
      • ►  Desemba (22)
      • ▼  Novemba (79)
        • Treni ya Umeme Kutumia Umeme Wake sio Unaokatika
        • Jeshi la Uganda lafanya mashambulio ya anga dhidi ...
        • KASSIM MAJAALIWA - Acheni Kutorosha Madini Nje Ya ...
        • Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Novemba 30
        • VIDEO KUBWA INAYOSUMBUA MITANDAO YA KIJAMII, ALIYO...
        • "Mume Wangu Kuwa Chawa sio Tatizo ili Mradi Alete ...
        • Kinachosubiriwa Kesi ya Kina Mbowe leo
        • HABARI ZA MAGAZETINI LEO NOVEMBER.29.2021
        • Rais Samia Ateua Viongozi Mbalimbali
        • Coco Beach ya boreshwa, Eneo la mihogo ya kukaanga...
        • SEREKALI YATOA TAMKO JINSI YA KUJIKINGA WIMBI LA 4...
        • Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Novemba 28
        • Makonda aburuzwa mahakamani, kesi Desemba 3
        • Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Novemba 27
        • Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Novemba 26
        • RPC Wankyo- Silaha 24 Zasalimishwa Pwani, Watu 21 ...
        • Uwekezaji Kwenye Dagaa Ni Muhimu Kiafya Na Kiuchumi
        • Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Novemba 25
        • Mrembo Aliyejioa Sasa Ajipa Talaka Baada ya Kupata...
        • Serikali Yapokea Dozi 499,590 Za Pfizer
        • Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Novemba 24
        • Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Novemba 23
        • Rais Samia atunuku Nishani na Shahada kwa Wahitimu...
        • Marefa Sasa Watafukuza Watazamaji Ligi Kuu Bara
        • M Dog Afunguka "Tumpongeze Diamond Platnumz ila An...
        • KIKAO CHA TACOSA, UMOJA WA WATANZANIA WANAOISHI AF...
        • HABARI MAGAZETINI LEO, 20 NOVEMBER 2021
        • Majizzo "Sio Davido Aliyembeba Diamond Platnumz Ba...
        • BREAKING NEWS: MOTO MKUBWA WAUNGUZA HOTEL ZA KIFAH...
        • HABARI MAGAZETINI LEO 18 NOVEMBER 2021
        • Rais Mwinyi atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Taasis...
        • Balozi wa TZ Afrika Kusini na Mkurugenzi Rutageruk...
        • Rais Kenyatta Amfuta Kazi Mkuu wa Magereza Kenya B...
        • Rufaa ya Lengai Ole Sabaya na Wenzake Kutajwa Dise...
        • Tanzania Hutumia Nusu Trioni Kuagiza Mafuta Ya Kula
        • Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Novemba 16
        • Marioo Aungana na Eric Omondi "Awapa Makavu Wasani...
        • Mpya Kabisa..Aliyekua Mpenzi wa JUX.. Jackline Cli...
        • Lukuvi "Marufuku Madalali Kuchukua Kodi ya Mwezi M...
        • Mahakama yatupa pingamizi kesi ya Freeman Mbowe na...
        • HABARI ZA MAGAZETINI LEO TAREHE 16 NOVEMBA 2021
        • HABARI ZA MAGAZETINI LEO TAREHE 15 NOVEMBER 2021
        • HABARI ZA KWENYE MAGAZETINI LEO 13 NOVEMBER 2021
        • Mbunge Aangua Kilio Bungeni
        • Kesi ya Mbowe: Shahidi Akutwa na Simu & ‘Diary’ Ki...
        • Rais wa Shirikisho la Soka Kenya Nick Mwendwa Akam...
        • Mahakama Yawaachia Huru aliyekuwa mhasibu wa Taasi...
        • Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Novemba 12
        • Mwanafunzi Aliwa na Mamba Akiogelea
        • Watanzania 725 Wafariki kwa Corona
        • Waliofukuzwa CUF sasa kushitaki kwa Msajili
        • Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Novemba 11
        • Bei Kubwa Vifurushi vya Data Tanzania Mwiba wa Mae...
        • HABARI ZA MAGAZETINI LEO TAREHE 10 NOVEMBA 2021
        • Kesi ya mtoto aliyefanya mtihani wa la 7 gerezani ...
        • HABARI ZA MAGAZETINI LEO, TAREHE 9 JUMANNE
        • TMA yatabiri ongezeko la joto kali nchini
        • MKUTANO MKUBWA WA KUFUNGA MWAKA UMOJA YA WATANZANI...
        • Jenipha Kanumba "Bikira Yangu Nimekutunzia Patrick...
        • Mange Kimambi Amlipua Paula "Paula Hasomi Turkey M...
        • Ukame na Njaa Tatizo Tena Kaskazini Mwa Kenya
        • Wabongo Hawana Dogo, Wamiminika Kwenye Page ya Koc...
        • HABARI ZA KWENYE MAGAZETINI, LEO JUMATATU NOVEMBER 8
        • HABARI MAGAZETINI LEO NOVEMBER 6
        • Ruby "Kusah Akiweka Mazingira Sawa Tutalea Wote Mt...
        • Watumishi waliogushi vyeti wapigwa ‘stop’
        • Bila Kujitoa Kwa Jasho na Damu Mtu Wangu Huwezi Ku...
        • Kenya yatangaza kupiga mnada ndege 73 za mataifa h...
        • Ndugai: Watanzania Wanalalamikia Mfumo wa Elimu
        • Askari wa Msumbiji washutumiwa kuwanyanyasa raia
        • Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Novemba 4
        • Mwanasheria wa Tigo atoa ushahidi kesi ya Freeman ...
        • HABARI ZA MAGAZETINI LEO 03 NOVEMBER 2021
        • RAIS MWINYI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI HOTELI YA ...
        • vitu ambavyo vinaweza kukufanya kuonekana mzee kul...
        • Shahidi aeleza kutowatambua watu kwenye CCTV kamer...
        • Amos Makala Atoa Ripoti "Wamachinga Dar Wamepanga ...
        • Huyo Ndio Mrithi wa Maalim Seif ACT WAZALENDO
        • Watu 690 wauawa Simiyu
      • ►  Oktoba (66)
      • ►  Septemba (129)
    • ►  2016 (187)
      • ►  Septemba (1)
      • ►  Juni (1)
      • ►  Mei (109)
      • ►  Aprili (57)
      • ►  Machi (19)
    • ►  2015 (738)
      • ►  Novemba (40)
      • ►  Oktoba (16)
      • ►  Septemba (6)
      • ►  Agosti (305)
      • ►  Julai (323)
      • ►  Juni (48)

    Videography and Photography

    Videography and Photography

    Wikipedia

    Matokeo ya utafutaji

    Created By SoraTemplates | Distributed By Gooyaabi Templates
    Inaendeshwa na Blogger.