Serikali yatangaza Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano Mwaka 2022
OFISI ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Baraza la Mitihani la Tanzania imekamilisha zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano katika shule za sekondari, Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Elimu ya Ufundi vya Serikali Mwaka 2022.
Zoezi hilo limefanyika kwa kuzingatia takwimu za matokeo ya wanafunzi waliofanya Mtihani wa Kidato cha Nne Mwaka 2021 kutoka Tanzania Bara.
==>>BOFYA HAPA KUTAZAMA MAJINA ( Awamu ya Kwanza)
Hayo
yamesemwa leo Mei 12,2022 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI),Mhe. Innocent Bashingwa (MB)
wakati akitangaza matokeo hayo ofisi ndogo za wizara jijini Dar es
Salaam.
Amesema,watahiniwa katika mtihani wa Kidato cha Nne kwa
mwaka 2021 waliopata Daraja la I hadi III walikuwa 173,422 wakiwemo
wasichana 75,056 na wavulana 98,366.
Kati ya wanafunzi hao,
wanafunzi wenye sifa ya kujiunga na Kidato cha Tano, vyuo vya Ualimu na
vyuo vya Ufundi ni 167,515 wakiwemo wasichana 71,433.
"Idadi hiyo
ya wanafunzi wenye sifa imejumuisha wanafunzi wenye mahitaji Maalum 508
wakiwemo wasichana 217 na wavulana 291. Hii ni ongezeko la wanafunzi
19,388 kwa kulinganisha na wanafunzi 148,127 waliokuwa na sifa kwa mwaka
2021.
==>>BOFYA HAPA KUTAZAMA MAJINA ( Awamu ya Kwanza)
Walikotoka
Mheshimiwa
Bashungwa amesema, wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano
na Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Elimu ya Ufundi mwaka 2022, ni kutoka
Shule za Serikali, zisizo za Serikali, watahiniwa wa kujitegemea
waliofanya mtihani kupitia Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima waliokidhi
vigezo na waliosoma Nje ya nchi ambao matokeo yao yamefanyiwa ulinganifu
wa Baraza la Mtihani Tanzania (NECTA).
"Wanafunzi 153,219
wakiwemo wasichana 67,541 na wavulana 85,678 sawa na asilimia 91.8 ya
wenye sifa, wamechaguliwa kujiunga na Shule za sekondari Kidato cha
Tano, Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Elimu ya Ufundi mwaka, 2022 katika
mchanganuo ufuatao;
"Wanafunzi 90,825 wakiwemo wasichana 43,104
wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano katika Shule za Sekondari 499
za Serikali zikiwemo Shule mpya 22 za Serikali zilizoanza mwaka, 2022.
"Kati
ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha Tano, wapo wanafunzi
wenye Mahitaji Maalum 481 ambao kati yao wasichana ni 204. Kati ya
wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, wanafunzi 41,401
wakiwemo wasichana 17,390 watajiunga kusoma tahasusi za Sayansi na
Hisabati na wanafunzi 49,133 wakiwemo wasichana 25,508 watajiunga kusoma
tahasusi za masomo ya Sanaa, Lugha na Biashara;
==>>BOFYA HAPA KUTAZAMA MAJINA ( Awamu ya Kwanza)
Fani mbalimbali
"Wanafunzi
1,880 wakiwemo wasichana 757 wamechaguliwa kujiunga na fani mbalimbali
katika Vyuo 03 vya Elimu ya Ufundi ambavyo ni Chuo cha Ufundi cha Arusha
(ATC), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na Chuo cha Usimamizi
na Maendeleo ya Maji (WDMI),"amefafanua Mheshimiwa Bashungwa.
Amesema,wanafunzi 2,294 wakiwemo wasichana 1,127 wamechaguliwa kujiunga na Vyuo vya Afya ngazi ya Stashahada;
Pia
amesema,wanafunzi 2,674 wakiwemo wasichana 1,366 wamechaguliwa kujiunga
na Vyuo vya Ualimu ngazi ya Stashahada ya Sayansi, Hesabu na TEHAMA.
Wanafunzi
6,457 wakiwemo wasichana 3,168 wamechaguliwa kujiunga na Astashahada ya
Elimu Maalum, Awali, Michezo, Msingi na Ualimu wa Shule zinazofundisha
kwa kutumia Lugha ya Kiingereza (English Medium).
Amesema,wanafunzi
49,089 wakiwemo wasichana 18,019 wamechaguliwa kujiunga na kozi
mbalimbali za Astashahada na Stashahada (Certificate and Ordinary
Diploma) katika Vyuo vya Elimu ya Ufundi vinavyosimamiwa na Baraza la
Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTVET).
Ongezeko
"Kwa
kuangalia takwimu za mwaka 2022, kumekuwa na ongezeko la wasichana 7,555
waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi
ukilinganisha na mwaka 2021.
"Hata hivyo idadi hii bado ni ndogo kulinganisha na wavulana,"amesema Mheshimiwa Waziri.
Mheshimiwa
Bashungwa amesema,ili kukabiliana na changamoto hii, wizara inaendelea
kuboresha miundombinu ya shule ili kuhakikisha wasichana wengi zaidi
wanajiunga na Kidato cha Tano.
"Aidha, tunachukua nafasi hii
kumshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa kuwezesha ujenzi wa shule za wasichana kumi (10) za mikoa
ambapo kila shule itachukua wanafunzi wapatao mia tatu (300) kuanzia
mwaka 2023.
==>>BOFYA HAPA KUTAZAMA MAJINA ( Awamu ya Kwanza)
14,254 wakosa nafasi
"Pamoja
na kuwepo kwa ongezeko la wanafunzi waliojiunga na Kidato cha Tano,
Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Elimu ya Ufundi kwa mwaka 2022, jumla ya
wanafunzi 14,254 wakiwemo wasichana 3,901 na wavulana 10,353 wamekosa
nafasi.
"Kati yao, wanafunzi 12,876 wana sifa ya kujiunga na
kidato cha Tano. Hali hii imetokana na ongezeko kubwa la wanafunzi
waliofaulu na waliokuwa na sifa ya kujiunga na Kidato cha Tano na vyuo
vya ufundi pamoja na ufinyu wa nafasi za Kidato cha Tano na Vyuo vya
Elimu ya Ufundi (NACTVET).
"Wanafunzi hao wanatarajiwa kujiunga
na kidato cha Tano katika awamu ya pili baada ya ukamilishaji wa baadhi
ya miundombinu ya shule na vyuo,"amesema.
Wito
Mheshimiwa Waziri Bashungwa amesema, muhula wa kwanza kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano utaanza Juni 13, 2022.
Hakuna maoni