Licha ya Kufukuzwa Chadema Kina Mdee Watinga Bungeni
Dodoma.
Baadhi ya wabunge kati ya 19 waliofukuzwa uanachama na Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakiingia bungeni tayari kuendelea na
shughuli za Bunge jijini Dodoma, leo Ijumaa Mei 13, 2022.
Jumatano
ya Mei 11, 2022 Baraza Kuu la Chadema lilitupilia mbali rufaa za
wabunge hao 19 kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho kuwafukuza
uanachama kwa tuhuma za usaliti kwa kukubali kwenda kuapishwa kuwa
wabunge kinyume na msimamo wa chama hicho kupinga matokeo ya Uchaguzi
Mkuu wa 2020.
Mbowe: Na wao waache uhuni
Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe amewajibu Halima Mdee na wenzake 18 kuhusu
uamuzi uliofanywa usiku wa kuamkia leo na Baraza Kuu la chama hicho,
waliouita wa ‘kihuni’, akiwataka na wao kuacha uhuni. Soma zaidi
Halima Mdee: Kilichotokea ni uhuni
Aliyekuwa
mwanachama wa Chadema, Halima Mdee amesema hakukuwa na uhuru kwa
wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho katika upigaji wa kura na kwamba,
kilichofanyika ni uhuni. Soma zaidi
Hakuna maoni