Rais Samia kufanya ziara ya siku mbili Uganda

Rais
Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya kiserikali ya siku
mbili nchini Uganda kuanzia leo Jumanne Mei 10 -11, 2022, kwa mualiko wa
Rais wa nchi hiyo, Yowei Museveni.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus
imeeleza kuwa madhumuni ya ziara hiyo ni kuimarisha na kudumisha zaidi
historia iliyopo na mahusiano ya kidiplomasia pamoja na ushirikiano wa
kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizo mbili.
Imeeleza kuwa katika
ziara hiyo, wanatarajiwa kujadili kuhusu masuala ya nishati, biashara,
usafiri, maendeleo ya miundombinu pamoja na sekta za afya.
“Hii
itakua ni ziara ya kwanza ya kiserikali nchini kufanywa na Rais Samia
tangu Serikali ya Awamu ya Sita iingie madarakani mwezi Machi 2021”
imeeleza taarifa hiyo.
Hakuna maoni