Breaking: Mahakama Kuu Arusha Yamuachia huru Lengai Ole Sabaya na Wenzake Wawili
Mahakama
Kuu ya Kanda ya Arusha leo Mei 6, 2022 imemuachia huru aliyekuwa DC wa
Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili waliokuwa wamekata rufaa ya
kupinga kuhukumiwa miaka 30 kwenda jela kila mmoja kwa sababu mbalimbali
.
Jaji
aliyekuwa akisikiliza rufaa hiyo, Ezedekia Kisanya amesema kulikuwa na
mkanganyiko kwenye mwenendo wa usikilizwaji wa kesi hiyo ikiwemo
kutofautiana kwa mashahidi na kuufanya ushahidi kuwa batili.
Hata hivyo, Sabaya ataendelea kukaa mahabusu kutokana na kukabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.
Hakuna maoni