Tanzanian Derby, Brown F.C vS Jumba F.C. 31/10/2021

Hii ni zaidi ya Derby ambaya inajumuisha wabongo kutoka Makao makuu ya Serekali ya South Africa ( Pretoria) wanao itwa BROWN F.C.


Ambao watashindana nguvu na vijana wenzao kutoka jiji la Johannesburg Kusini(Turfforntain), Jiji la kimataifa la biashara na maujanja yote Nchini Afrika ya Kusini JUMBA F.C.

Mechi hiyo inatarajiwa kuwa yenye ushindani mkubwa, kwani JUMBA F.C anatarajiwa kusafiri kutoka Jiji la Johannesburg kuelekea Pretoria kama wageni ilikuweza kukipiga..

Huku BROWN F.C. watakuwa kwenye uwanja waobwa nyumbani unaoitwa SOUTPAN GROUND GEZINA PRETORIA..
Siku ya Tarehe 31/10/2021.

Hii sio mechi ya kukosa kwa yeyote mpenda michezo, na mpenda kujichanganya na Watanzania na ndugu wote kutoka mataifa mbalimbali.

Kazikazi Media watakuwepo siku hiyo kuweza kutoa habari zote kwa kila kilichotokea, na matokeo ya mchezo huo wa watani hao.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.