HONGERA TWIGA STARS
Kwa niaba ya Watanzania wote waishio Afrika Kusini, tunatoa pongezi zetu za dhati kwa timu yetu ya Taifa ya wanawake *TWIGA STARS* kwa kushinda kombe la COSAFA.
Tunawapa pongezi wachezaji wote, makocha, kamati zote za ufundi na maandalizi kwa mafanikio haya makubwa kwa taifa letu Tanzania.
Pia pongezi kwa balozi wetu Meja Jenerali Gaudence Milanzi na ubalozi kwa mapokezi na kuwapa moyo timu yetu na wametimiza yote uliyowaambia ambalo ni kuchukua ubingwa wa COSAFA 💪👏
Kwa kweli mmeshinda katika mazingira magumu bila washabiki ila mmeweza kututia katika ramani ya michezo barani Afrika na duniani kwa ujumla.
Hongera sana
Kwa niaba ya Watanzania wote waishio Afrika Kusini.
Alex Minja
Katibu TACOSA
9 October 2021
Hakuna maoni