WEMA SEPETU: Hata Kama Nikizeeka Nyota Yangu itabaki Pale Pale Japo Kuna Watu Wanatamani izimike
Nyota na ing’ae! Mtoto mzuri Bongo, Wema Isaac Sepetu ameliambia Ijumaa
Wikienda kuwa hata kama akizeeka na kuwa kikongwe, bado nyota yake
itaendelea kung’aa siku zote wala haitafifia kwani amezaliwa nayo labda
asiwepo duniani.Wema ameliambia gazeti hili kuwa anamshukuru Mungu kwa kumjalia nyota hiyo ambayo inawezekana kuna watu wanatamani izimike wakati wowote, jambo ambalo haliwezekani leo wala kesho na kwa kuwa alitoka nayo tumboni kwa mama yake, Miriam Sepetu.
“Hata kama watu wataichafua kiasi gani, nyota yangu itaendelea kung’aa hadi nitakapokuwa mzee. Nitakuwa ni bibi mwenye mvuto na hata watoto watapenda kusikiliza hadithi zangu,” alisema Wema
Hakuna maoni