‘Cinderella’ ya Ali Kiba iliuza Mil. 200, matumizi je? swali la ‘Kidoti’? Haupendi wimbo wake? Majibu haya..

Kwenye show ya XXL alhamisi ya November 12 2015 mgeni aliyealikwa alikuwa ni Ali Kiba ambaye alikuja kuzindua mdundo wa ngoma mpya ambayo wameshirikiana na Christian Bella… lakini kuna story za zamani hivi nazo ziliguswa pia.
Unajua Ali Kiba akiisikia ngoma ya ‘Usiniseme’ anakumbuka wapi? >>> ‘Nakumbuka safari zangu kwenda G Records, ilikuwa ni lazima niende nikashinde na Producer wangu KGT kila siku hata kama sina kazi‘- Ali Kiba.
Ana mpango wa kuachia album? >>> ‘Nitatoa album mwakani kwa mfumo wa digital nikimpata msambazaji mzuri… nataka kufanya album kali sio nijaze tu nyimbo kwenye album… nakumbuka album ya kwanza niliyonunua ilikuwa album ya AY, halafu nikanunua ya Matonya… ni kuonesha tu kwamba najali muziki…’- Ali Kiba.
Ali K II
Ali Kiba aliachia album ya Cinderella mwaka 2009, anajiona wapi toka mwaka huo >>> ‘Najiona kama kiwango changu kimekua sana… sipendi wimbo wa ‘Shababi’ kwa sababu najiona niliimba chini ya kiwango
Ali Kiba II
Mauzo ya Cinderella je? Matumizi yake? >>> ‘Cinderella ilivunja rekodi na sijawahi kusikia kama kuna album nyingine iliwahi kuizidi mauzo… iliuza nakala milioni mbili, kila copy nilikuwa nachukua shilingi 200… jumla inakuwa kama Mil. 200 hivi sema wakati ule utoto mwingi ila nilifanikiwa kujenga.’
Ali K III
Presenter wa XXL, Adam Mchomvu akachomekea swali kuhusu Kidoti, majibu yaliyotoka ni haya hapa >>> ‘Mjasiriamali, bishosti kanyooka, yuko fresh… yap… full stop‘- Ali Kiba.
Sauti ya Ali Kiba hii hapa niliyorekodi show ya XXL leo November 12 2015

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.