MWILI WA MTANZANIA ABDUL (SUGU), WAAGWA NA KUSAFIRISHWA USIKU WA LEO



                              

Tukiongea na kiongozi wa watanzania nchini afrika ya kusini kwa njia ya Simu, Kuhusu maswala ya Mtanzania Abdul (Sugu) alisema wameshafanikiwa kuufanyia mwili wa marehemu sugu vipimo vya kutambua nini chanzo halisi cha kifo chake (Postmortem) kwenye Private Hospital, Na kuambiwa majibu yatatoka baada ya wiki moja, ili tuweze kufungua kesi ya mauwaji dhidi ya ndugu yetu.

Hivyo ilibidi wa uchukue mwili wa marehemu na kuendelea na taratibu za mazishi, Mwili wa marehemu Abdul Sugu, Unatarajiwa unafanyiwa taratibu za kusafirishwa nyumbani Tanzania, Leo Jioni na utawasili nyumbani Tanzania Usiku wa saa 8 Siku ya Ijumaa Tarehe 21/01/2023.


Wamefanikiwa kuuswalia mwili wa marehemu huyu kwenye msikiti wa Myfair, Asubui ya leo na umati wa watanzania na mataifa mengine walijitokeza kwa wingi kuweza kumsindikiza kijana huyu wa kitanzania aliouwawa na polisi, kwa kufananishwa kama wasemavyo watu wa karibu walio kuwa karibu siku ya tukio.


Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.