Prince Harry: "Kwa mara ya kwanza nililala na mwanamke kwenye majani"

Siku chache zilizopita toto tundu, Mwanamfalme Harry amezindua kitabu chake kinachoitwa Spare. Kitabu hicho kimekuja wiki chache baada ya kutoka kwa filamu ya maisha yake pamoja na mkewe. Katika kitabu hicho, Prince Harry ameeleza mambo yaliyotokea katika maisha yake mengine ya kuhuzunisha na mengine ya kufurahisha. Prince Harry ameeleza maisha yake vitani huko Afghanistan. "Nikiwa vitani niliuwa wanamgambo 25", anaandika Prince Harry. Pia Harry ambaye kwa macho ya wengi anaonekana kama mtukutu ameeleza jinsi kaka yake alivyompiga na kumgalagaza chini. Ugomvi huo ulianza baada ya Prince William kumuita Meghan Markle, mke wa Prince  Harry  kuwa ni mtu mgumu, mkorofi na mpenda ugomvi. Mvutano ulikuwa mkali mpaka Kaka yangu "akanikwida na kuniangusha chini". 

Kwenye kitabu hicho Prince Harry ameeleza jinsi baba yake, Mfalme Charles alivyo wahi kutania inawezekana kuwa, yeye sio mtoto wake labda ni wa mchepuko wa mama yake aliyekuwa anaitwa Major James Hewitt. Prince Harry anasema hakupendezwa na utani huo  kwa sababu huko mtaani watu walikuwa wanajua mahusiano ya mama yake Princess Diana na Major James. Katika mahojiano na BBC, Princess Diana alikiri kuwa na mahusiano na msaidizi wake Major James Hewitt, hata hivyo mahusiano hayo ya kimapenzi yaliyodumu  kwa miaka mitano yalianza miaka miwili baada ya Prince Harry kuzaliwa.  Katika maisha yake ya ujana na mwanzo wa mahusiano yake ya kimapenzi, Prince Harry ameeleza kwamba mwanamke aliyefanya naye mapenzi kwa mara ya kwanza alikuwa mkubwa kuliko yeye. Prince Harry anaandika, "....yule mwanamke alikuwa mkubwa kuliko mimi, na kibaya zaidi nililala  naye kwa mara ya kwanza kwenye majani, nyuma ya bar "....nyie nitawauliza siku nyingine, siku ya kwanza ilikuwa wapi, ila ndugu zangu huko Musoma ni kwenye majani tu kama Harry...C&P

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.