MTANZANIA AUWAWA NA POLISI LEO KWA KUVALISHWA MFUKO KICHWANI JOHANNESBURG AFRIKA YA KUSINI

Kwa habari za harakaharaka zilizotufikia mtanzania mkazi wa Johannesburg afrika ya kusini maarufu kwa jina la Abdi Sugu, aliekuwa anaishi maeneo ya Fox Street Johannesburg.

Wakiongea jamaa zake wa karibu na watu walikuwa karibu na tukio "Wanasema marehemu sugu alikuwa akiwindwa na mapolisi kwa kufananisha au kwa kuchomeshwa na wabaya(snich) zake kuwa atakuwa na madawa au pesa nyingi taslimu, hivyo siku ya jumapili 15/1/2023 Usiku alitoka out kujirusha maeneo ya kujidai Club, mida ya saa 4 usiku.

Huku nyumbani Kumbe kulikuwa na Tag la polisi waliokuwa na gari(Private) yenye namba za kiraia (private) wakiwa wamepaki eneo la tukio, wakiwa wanasubiria marehemu Sugu atokea au aingie nyumbani kwake, Mpaka mida ya saa8 za usiku umeme ulipokatika ndio marehemu alishuka kwenye Tax/Uber nakuelekea kwenye flat ya mjengo anako ishi.. wakati anaingia ndipo kundi la polisi walipo mvamia na kuanza kupiga na kuanza kumuuliza wapi pesa zilipo marehemu sugu aliwapa kiasi kilichokuwepo lakini bado walionekana kutaka zaidi ndipo walipoanza kumpiga kwa kumtesa na ndipo raia na majirani wakasikia makelele ya kulala mika, marehemu sugu akisema wananiuwa wananiuwa..

Waliendelea kumpiga na walipoona marehemu hayuko tayari kuwapa ushirikiano na kulikuwa kumeshaanza kupambazuka mida ya saa 10alfajiri, marehema walimvalisha mfuko kichwani huku wakiendelea kumpiga na kumtesa, ilipofika mida ya 11asubui na watanzania walikuwa wameshapeana taarifa kuwa anaepiga makelele ni ndugu yao Sugu.. walianza kufanya fujo na kuanza kurusha mawe na kuanza kuwapiga polisi waliokuwa na ndugu yao huyo, wakati vita hiyo inaendelea polisi walikuta mtanzania huyo ameshafariki dunia ndani ya plastic bag hiyo,  Ndipo walibidi waite gari yakubebea mwili mida ya saa 12:30 asubui kuja kuubeba mwili wa matehemu Abdul Sugu..

Ilipofika saa 1asubui siku ya leo jumatatu 16/1/2023 kulikuwa na kuja isiosemekana kati ya watanzania na mapolisi wa Afrika ya kusini"
(Alimalizia na hivyo ndugu msimuliaji ambae aligoma kutaja jina lake kabisa)

Mpaka muda naondoka eneo la tukio polisi wapo kila kona na silaha na magari ya maji ya kuwasha na ya kubebea watu (matenga & kumbakumba)

Nikiriporti kutoka Johannesburg eneo la tukio FOX ni mimi mwandishi mchapa kazi.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.