MAJONZI YA TAWALA AFRIKA YA KUSINI: Kifo cha MTANZANIA ndugu William Moses Mpangala wa (TACOSA)
TANZIA TANZIA TANZIA
Habari ndugu zangu wanachama wa TACOSA na Watanzania wote kwa ujumla.
Kwa masikitiko makubwa natangaza kifo cha mwanachama na kaka yetu William Moses Mpangala kilichotokea jana jioni (08 January 2023 huko nyumbani kwao Mheza, Tanga, Tanzania.
Kama tunavyokumbuka ndugu yetu alisafiri siku ya Alhamis iliyopita na alifika nyumbani salama na akaendelea na matibabu. Jana aliamka akiwa na nguvu na alishinda akiongea na mama na ndugu zake kwamba anashukuru amefika na atapona tu, jioni alijisikia kidogo amechoka na alisimama kuingia bafuni na ndio umauti ulimkutia huko😭🙆🏻♂️
Kwa niaba ya uongozi wa TACOSA na Watanzania wote tunawapa pole familia ya kaka yetu na kumtakia pumziko la Amani huko aendako. Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe 🙏
Tumepoteza mwanachama mwingine katika muda mfupi ndugu zangu na wanachama wenzangu naomba tumuombe Mungu atulinde na mbaya na Vilevile tuiombee familia katika wakati huu mgumu 🙏
Maandalizi ya mazishi yanaendelea na tutatoa taarifa kamili baada ya kuzipata🙏
Pamoja na yote mama na ndugu wa kaka yetu wanatoa shukrani za kipekee kwa umoja wetu kuhakikisha ndugu amefika nyumbani na umauti umemfika baada ya kuwaona ndugu zake🙏
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya kaka yetu mahala pema peponi.🙏
Mungu amjalie kauli thabiti
JibuFuta