Balozi wa Watanzania Afrika ya kusini akutana na viongozi wa Jumuiya za watanzania waishio nchini Afrika ya kusini Leo





Leo tarehe 4 Machi,2023, Kiongozi wa Watanzania mwenye dhamana ya kuiwakilisha Serekali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini Afrika ya Kusini, Mhe.Maj. Gen.(Mst) Glaudence Milanzi,  ameitisha mkutano na Viongozi wote wa Jumuiya za Watanzania  wanaoishi nchini Afrika ya kusini,Botswana na Lesotho. Mkutano huo umefanyikia Ubalozi wa Tanzania uliopo jijini Pretoria nchini Afrika Kusini.

Lengo la mkutano huo pamoja na masuala mengine ni kujadili maswala mbalimbali na changamoto zinazowakabili Watanzania kwenye maeneo wanayoishi na kuzitafutia suluhisho la pamoja.Vilevile ameitisha mkutano huo ili  kujadiliana namna ya kuweza kuwasaidia raia wa Kitanzania kwa  kuwashauri kufuata sheria,taratibu na kanuni zilizowekwa na Mamlaka za maeneo wanayoishi  ili kuweza kuboresha maisha yao  kwenye maeneo wanayoishi.


Itakumbukwa kuwa, huu sio mkutano au vikao vya  kwanza kuitishwa na Mhe. Balozi Milanzi. Katika mwaka 2022 takribani  vikao16 vilifanyika Ubalozini,Johannesburg, Pretoria,Capetown, Botswana na Lesotho. Kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2023 kwa nyakati tofauti tayari Ubalozi umeitisha vikao  takribani vinne kwenye miji ya Kwa Zulu Natal,Eatesrn Cape (PE) na Pretoria.

Mhe. Balozi Milanzi  pia amewaomba viongozi hao kuwahimiza Watanzania walio kwenye jumuiya zao wasio na kazi maalumu kwenye maeneo waliyopo kurejea nyumbani Tanzania kwani mazingira ya uchumi yamefunguka na fursa zipo katika utawala wa sasa chini ya Mhe. Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan. Aidha, amewaomba Watanzania hao kujisajili Ubalozini ili kuuwezesha Ubalozi kuwa na taarifa zao ili uweze kuwasaidia punde watakapohitaji msaada wa Ubalozi. Pia, amesisitiza mshikamano na ushirikiano baina ya diaspora wenyewe kwa wenyewe na Ubalozi pindi  kutakapokuwa na shughuli za Kitaifa na za kijumuiya zitakazoandaliwa na diaspora hao.

Maoni 2 :

  1. Kazi nzuri

    JibuFuta
  2. Hongera Sana kiongozi kwa kazi njema, Lakini pia hongereni mliofanikiwa kufika kwenye kikao. Asanteni Sana kwa kazi njema Mungu wa mbinguni awabariki Sana.

    JibuFuta

Inaendeshwa na Blogger.