WANANCHI WA BONDE LA MTOMSIMBAZI, WAOMBA MKUTANO NA SEREKALI KUPITIA TAMISEMI, WAELEWESHWE MASWALA YA FIDIA ZAO KUWA NA TATHMANI NDOGO
Kazikazi Media Tukiwasiliana kwa Njia ya Simu na Kiongozi na muwakilishi wa Wakazi wa bonde la msimbazi ndugu Godfrey Carthbert "Amesema wakazi wa bonde la msimbazi wamekuwa kwenye wakati mgumu baada ya kupewa tathmini zisizo weza hata kuwajengea nyumba yenye hadhi waliyokuwa wanamiliki wakiwa kwenye maeneo yao waliopo sasa bondela msimbazi, Maana pia ujenzi kwa sasa umepanda na hali ya maisha pia imepanda mno.
Hivyo wana omba mkutano na viongozi wao na wawakilishi wao serekalini , waheshimiwa Wabunge wao, madiwani, Mawaziri na Wasimamizi wa Mradi huo TAMISEIMI iliwaweze kuongelea swala lao la Fidia, je Walitumia njia gani kufanya mahesabu mpaka kuweza kuwalipa wananchi hao million 2 kwa mwananchi mmiliki wa nyumba ya vyuma vitatu, au mmiliki wa nyumba kubwa na yenye mabanda ya uwani 6 kumpa milioni 17 au milioni 22. Wananchi na wapiga kura wanaomba kufahamu majibu Serekali na World bank walitenga kiasi gani kwa fidia hiyo.
MAELEZO KAMILI TAZAMA VIDEO HAPO CHINI......
Hakuna maoni