WAKAZI WA BONDE LA MSIMBAZI WALALA MIKIA SEREKALI NA MRADI WA WORLD BANK, KWA KUWALIPA FIDIA NDOGO INAYOWAPELEKEA KWENYE UMASIKINI
DMDP - Dar es Salaam Metropolitan Development Project Huo ndio Mradi uliofadhiliwa na WORLD BANK(Bank ya Dunia) kwa asilimia 100% ilikuweza kufanya haki ya malipo kwa wakazi na wamiliki wa maeneo yatakayo guswa na mradi huo wa Bank ya Dunia ilitoa fungu maalumu la Pesa ilikuweza kuwalipa Fidia wananchi wake pamoja na Pesa za kuwahamisha, kodi na Kifuta jasho watakazo Walipa ilikupisha mradi ufanye kazi. Kitu cha kushangaza ni kwenye fidia imekuwa ndogo kiasi kwamba wameshindwa hata kupata haki ya kupata pesa ya kununulia au hata kujengea nyumba ya kufanania, kitu ambacho kimeleta sinto fahamu kubwa na kuwafanya walipwaji kuona maradi huo sio rafiki kwao maana haujawatendea haki ikiwa wao ni rai wa Tanzania na iwaje wanakosa kutendewa haki ya kupokea pesa zinazostahiki thamani ya nyumba wanazomiliki maana wote walikua tayari kuondoka kama shwala lao la fidia litawatendea haki kama walivyokuwa wakiwataarifu kwenye vikao vya Maoni na Taarifa za mradi huu.
Ni kiongea kwa njia ya Simu na Viongozi wa Wakilishi wa Watanzania wenyemakazi yao na wanao miliki nyumba maeneo yote Kandokando ya MTO MSIMBAZI Jijini Dar es salaam, Katika Wilaya za ILALA na KININDONI, Ndugu Godwin Cathbert (Magomeni Sunaa) na Mama Madiba Mwanduma (Msimbazi) Hii ni baada ya malala miko mengi yaliotokea baada ya wananchi kutoku ridhishwa na Fidia ya kuwa hamisha kwenye makazi hayo kuwa lengo la kupanua na kuendeleza Jiji la Dar es salaam.
"Wakiongea kwa njia ya simu wameonekana kupokea malalamiko mingi 99% Wakazi wa Bonde la mtomsimbazi kutokupata haki yao na kutokuridhishwa na Utandaji wa Serekali na Bank ya Dunia, Kwa kusema hawajatendewa haki maana kwenye swala la fidia wamekuwa wakifanyiwa Interview kwa siri siri na malipo utakayolipwa ni kutokana na Utakavyo jielezea au kuburgen na watakao kulipa. Wengi wamesema walitegemea Uwazi zaidi kwenye malipo hayo kama walivyokuwa wakiwafanyia uwazi walipo waletea wazo la mradi na kuwashirikisha katika kila hatua, lakini kwa sasa imekuwa ndivyo sivyo wanalipa MILIONI KUMI NA NNE(14) kwa wenye nyumba ya vyumba 10, Na MILLIONI NANE(8) kwa nyumba ya vyumba 6. Kwa masikitiko makubwa wanasikitika na kuomba msaada kwa Kiongozi wa Vuu kulisimamia Hili swala lao, waweze kutendewa haki ijulikane katika nyumba zote elfu 2 benki ya Dunia walitenge pesa Billioni ngapi kwa ajili ya kuwalipa fidia ya kuwahamisha, maana uwamalipo ya milioni 14 au millioni 8, Na kwa jinsi hali ya maisha ilivyokuwa ni ngumu na ujenzi ulivyokuwa ngarama kwa sasa hii inawatia umasikini na hata kuwaletea kifo, maana wengi wao ni wamama watu wazima na wanawatoto na wajukuu, kweli haki inabidi itendeke ilituweze kuwaokoa watanzania na wananchi wa bondela msimbazi"
MAELEZO YA KIONGOZI KUHUSU MALIPO YALIVYO YALIOFANYIKA KINYUME NA MAZUNGUMZO KATI YA WAKAZI WA BONDE LA MSIMBAZI NA TAMISEMI GUSA VIDEO CHINI......
Hakuna maoni