Mhandisi Maryprisca Mahundi ametoa onyo hilo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mkula wilayani Busega wakati akikagua mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni mbili unaotekelezwa na Serikali kwa ajili ya kuhdumia wananchi wa vijiji vitano vya eneo hilo.

Amewataka watendaji hao kuanza kufanya kazi kwa pamoja ili kuleta tija na kudai kuwa tabia ya kuchafuana itasababisha halmashauri hiyo kuwapoteza viongozi wenye uwezo wa kuwasaidia wanancchi kupata maji.