Biden asema Putin hajui kinachokuja kutokea
Katika hotuba yake hiyo, Bwana Biden aliapa “uamuzi usioyumba kwamba daima uhuru utashinda dhidi ya udhalimu”.
Hotuba hiyo inakuja wakati Wamarekani wanaonekana kuchoshwa na janga linalowafanya kukabiliana na mfumuko wa bei.
Rais huyo wa chama cha Democratic aliwaambia wabunge Jumanne usiku: “Vita vya Putin vilipangwa na havina sababu. Alikataa juhudi za mara kwa mara katika diplomasia.
“Alidhani nchi za Magharibi na NATO zisingechukua hatua. Na, alidhani angeweza kutugawanya hapa nyumbani.
“Putin alikosea. Tulikuwa tayari.”
Bwana Biden alitangaza kuwa Marekani itapiga marufuku ndege za Urusi katika anga yake, kama zilivyofanya mamlaka za Canada na Ulaya.
Akisisitiza vikwazo zaidi vya kiuchumi dhidi ya Urusi, rais wa Marekani alisema kuhusu Putin: “Hajui nini kinakuja.”
Hakuna maoni