Beckham kumsajili Lionel Messi Inter Miami
Klabu ya David Beckham inayoshiriki ligi kuu ya Marekani ya MLS, Inter Miami ipotayari kufanya kila linalo wezekana kumsajili, Lionel Messi, 34 iwapo mchezaji huyo wa Argentina ataamua kuondoka Paris St-Germain mapema msimu huu.
Mchezaji huyo bora zaidi duniani, Lionel Messi bado hajaanza kuuwasha moto ndani miamba hiyo ya soka pale Ufaransa kama alivyoweza kufanya hivyo akiwa Barcelona.
Messi mpaka sasa amefunga jumla ya magoli 7 pekee kwenye michezo 23 aliyocheza kwa matajiri hao wa Jiji la Paris.
Hakuna maoni