“Ndugu yetu Mbowe leo yuko huru ameachiwa na kutokana na hilo nikaona kuna umuhimu wa kukutana naye leo ili tuzungumze mawili matatu, lakini kubwa tulilozungumza kwamba Tanzania ni yetu wote tunatakiwa kushirikiana.
“Na katika hilo muhimu ni kujenga kuaminiana kwa misingi ya haki na kwamba tunaposimamisha misingi hiyo; kuaminiana, haki na kuheshimiana ndiyo tutapata fursa nzuri ya kuendesha nchi yetu na kuleta maendeleo,” alisema Rais Samia.
Kwa upande wake, Mbowe alisema katika mazungumzo yao alimshukuru Rais Samia kwa kujali na kwa pamoja wamekubaliana kushirikiana ili kuhakikisha kwamba wanaliletea Taifa maendeleo.
“Namshukuru Rais kwamba ameridhia tukutane na nikaona ni jambo la msingi sana kuja kumwona Mheshimiwa Rais baada ya kuwa gerezani kwa kipindi cha takribani miezi minane. Nimemshukuru Rais kwa kuwa concerned (kujali),” alisema Mbowe.
Alisema wamezungumza mambo mbalimbali ambayo kwa muda mrefu yamekwaza uhusiano mwema kati ya chama tawala kinachoongoza Taifa na chama kikuu cha upinzani nchini.
“Tumekubaliana msingi mkubwa wa kujenga Taifa letu katika maridhiano na umoja unaokubalika, ni kusimama katika misingi ya haki na pale neno haki linapotawala basi amani inakuwa ni automatic (inakuja
“Kwa hiyo tumekubaliana kwamba tunahitaji sana kujenga katika Taifa letu na kila jambo ikiwemo Bunge na taasisi yoyote nyingine ya umma, vyama vya siasa, vyama vya upinzani, chama kinachoongoza, vyote viweze kuihubiri haki,” alisema Mbowe.
Alisisitiza kwamba ili kujenga misingi hiyo kuna umuhimu wa kuaminiana, kwa sababu wamekuwa na urafiki wa mashaka kwa muda mrefu. Alisema wanahitaji kusonga mbele kwa kufanya siasa za kistaarabu, za kiungwana, ili kuisaidia Serikali kufanya majukumu yake na Serikali nayo ihakikishe nao wanafanya majukumu yao vizuri.
“Sisi tumempa Mama hiyo assurance, (uthibitisho) naye amesema atatupa hiyo guarantee kwamba hayo yatafanyika na sisi tuko tayari kumpa ushirikiano na tunaomba ushirikiano kwa Watanzania wote, wampe ushirikiano, watupe ushirikiano, tuijenge nchi yetu,” alisema Mbowe.
Hali ilivyokuwa Mahakamani
Juzi wakati wa kuanza kwa kesi, mpaka saa 4:30 asubuhi washitakiwa walikuwa hawajafikishwa mahakamani.
Ilipofika saa 4:55 asubuhi, Mahakama ilianza ambapo wakili wa jopo la utetezi, Peter Kibatala aliieleza Mahakama kuwa yeye na mawakili wenzake walikuwa wameshajiandaa kwa ajili ya washtakiwa kuanza kujitetea lakini wamepokea taarifa kutoka kwa Ofisa wa Magereza kuwa, mshtakiwa wa nne, Freeman Mbowe ni mgonjwa.
Baada ya kueleza hayo, kiongozi wa jopo la mawakili wa Serikali, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando aliieleza Mahakama kuwa, hatajibu hoja ya Wakili Kibatala bali anaombi moja ambalo ni DPP kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Majira ya saa 8 mchana, msafara wa Mbowe ulitoka katika gereza la Ukonga ukiwa na magari mawili, moja likiwa ni Land Cruiser V8 alilopanda yeye na washtakiwa wenzake na lingine ni Pick-Up ya M4C iliyokuwa ikiendeshwa na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu akiwa na baadhi ya wanafamilia.
Msafara huo uliingia katika gereza la Segerea saa 8:30 alikokuwepo mshtakiwa Halfan Bwire na walikaa humo hadi ilipofika saa 10:40 jioni ambapo walianza kuelekea nyumbani kwa Mbowe maeneo ya Mikocheni.
Walifika Mikocheni saa 11 jioni ambapo watu mbalimbali walikuwepo nyumbani hapo wakimsubiri
Hakuna maoni