MAN CITY YAWEKA REKODI KUSHINDA MECHI NYINGI MWAKA MMOJA
MABINGWA watetezi, Manchester City wameendeleza ubabe katika Ligi Kuu ya England baadaya ushindi wa 4-0 dhidi ya Newcastle United jioni ya leo Uwanja wa St. James' Park, Newcastle upon Tyne. Mabao ya Manchester City yamefungwa na Ruben Dias dakika ya tano, Joao Cancelo dakika ya 27, Riyad Mahrez dakika ya 63 na Raheem Sterling dakika ya 86 huo ukiwa ushindi wa nane mfululizo na wa 34 mwaka huu kocha Pep Guardiola akiweka rekodi mpya ya kushinda mechi nyingi mwaka mmoja.
Manchester City wamevunja rekodi iliyowekwa na Liverpool chini ya kocha Bob Paisley kushinda mechi 33 mwaka 1982 na wanafikisha pointi 44 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi nne zaidi ya Liverpool baada ya timu zote kucheza mechi 18.
Hali ni mbaya kwa Newcastle United kwani wanabaki na pointi zao 10 baada ya mechi 18 katika nafasi ya 19 kwenye ligi ya timu 20, ambayo mwisho wa msimu tatu zitashuka daraja.
Hakuna maoni