LIVERPOOL PUNGUFU YATOA SARE NA SPURS 2-2 LONDON
WENYEJI, Tottenham Hotspur wamelazimishwa sare ya 2-2 na Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Tottenham Hotspur Jijini London.
Mabao ya Spurs yamefungwa na Harry Kane dakika ya 13 na Son Heung-Min dakika ya 74, wakati ya Liverpool yamefungwa na Diogo Jota dakika ya 35 na Andy Robertson dakika ya 69 kabla ya kutolewa kwa kadi nyekundu dakka ya 77 kwa kumchezea rafu Emerson Royal.
Liverpool inafikisha pointi 40 na kubaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi nne na mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 18, wakati Tottenham inatimiza pointi 26 za mechi 15 katika nafasi ya saba
Hakuna maoni