MWANAMKE ANAYEISHI NA WANAUME WAWILI AONGEZA MUME WA TATU, WENZAKE WAMPOKEA KWA VIFIJO NA NDEREMO.
Wakati unaendelea kushangaa ya Mchungaji Paul Mackenzie yanayoendelea huko nchini Kenya, ngoja nikusanue na hii nyingine.
Mwanamke wa Kimarekani aitwaye Kenya K Stenens ambaye anaishi na wanaume wawili kwa mpigo ameamua kuongeza mume wa tatu.
Kenya amemtambulisha mumewe huyo wa tatu mbele ya wanaume wake wawili ambao walimpokea na kumkaribisha kwa furaha.
Kenya ameolewa na mume wake wa kwanza kwa zaidi ya miaka 29, na wapili kwa zaidi ya miaka mitano na wote wamekuwa wakipata haki yao ya tendo la ndoa kwa wakati kila wanapohitaji.
Kenya anasema amekuwa akiifurahia zaidi ndoa ya wanaume wengi (Polyandry Marriage), hata hivyo watu wamebaki na minong'ono na maswali kwamba anawezaje kuwamudu njemba hao ambao wote wanaonekana ni watu wa gym mbavu nene.
Hakuna maoni