MKUTANO MKUU WA VIONGOZI WA JUMUIYA ZA WATANZANIA AFRIKA YA KUSINI, UTAFANYIKA 25 NA 26 NOVEMBA 2023
Hatima ule mkutano uliokuwa ukisubiriwa na watanzania waliokuwa wengi washio Afrika ya kusini, wenye lengo la kukutanisha viongozi wa majimbo mbalimbali ya Afrika ya kusini, unatarajiwa kufanyika ndani ya Jiji kubwa la Johannesburg, Siku ya Ijumaa na Jumamosi mfululizo yani tarehe 25 na 26 mwezi wa Novemba kwa lengo la Watanzania wote kuwa na chama kimoja na kuwana sauti moja ya kimipango na mikakati na katiba moja ya kuwaongoza.
Pia kuzitafutia ufumbuzi
Agenda na changamoto zifuatazo:
1. Viongozi wa Jumuiya/maeneo kukutana na kufahamiana ili kujenga
ukaribu na udugu
2. Jinsi
ya taasisi/jumuiya za Watanzania kufanya/kuamua mambo kwa umoja
3. Mapendekezo/mjadala wa katiba
itayounganisha jumuiya mbalimbali za
Watanzania
4. Changamoto za kijamii na njia bora na
kuzitafutia suluhisho la kudumu
(magonjwa,
Vifo na mazingira magumu ya maisha).
5. Maendeleo na Akiba ya uzeeni (Vibali
vya kuishi/kufanya kazi, biashara na
uwekezaji,
akiba na mafao ya uzeeni)
6. Uongozi
na maana yake (semina/lecture)
7. Waongeaji na watoa elimu wa janja
tofauti za maisha (kama watavyopatikana)
Tutakuwa na Ugeni kutoka
kwenye Ubalozini Pretoria, Na wakilishi/washirika wa kutoka
-Ben's Agrostar Tanzania
Ltd na Ben's Agrostar pty Ltd south
-CRDB Bank Tanzania
-Wizara ya Viwanda na
Biashara Tanzania
-Wizara ya Kilimo
-Shirika la Nyumba
Tanzania
-NBC Bank Tanzania
Eneo la Mkutano ni Houghton
School, 1st Avenue,
Houghton Estate,
Johannesburg 2198
Muda Ni kuanzia saa
2asubui mpaka 11jioni.
Wote
Mnakaribiswa kushiriki haswa Kama wewe ni mtanzania unakaribishawa
kuhudhuria, kwa kujua na hata kuleta kero ya changamoto.
kwa mawasiliano zaidi: Tanzanian Community in South Africa, 24 Barney Simon Street, Johannesburg, 2094, R.S.A Tel: +27 66 557 5454 Email: admin@tacosa.org.za Web: www.tacosa.org.za,
Hakuna maoni